Ismail Mapanga alikuwa mpiga gitaa bezi katika bendi ya msondo ngoma amefariki dunia usiku wa leo katika hospitali ya temeke , Ismail amefariki dunia kwa maradhi yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu kidogo, kwa mujibu wa bendi ya msondo ngoma, Ismail atazikwa leo mchana saa saba katika makaburi ya yombo, Mungu aulaze mwili wa marehemu mahala pema peponi amina.