Akiongea
na blog hii msanii wa muziki wa hip hop Bongo amesema kuwa video yake
mpya ya 2030 inakaribia kutoka hivi karibuni hivyo watu wakae mkao wa
kula kwasababu video hiyo inaeleza mambo mengi sana kuhusiana na maisha
halisi ya Tanzannia, Roma Mkatoliki ni msanii ambaye alisha chukuwa tuzo
2 za musick wa Hip Hop Bongo hivyo anapenda kuwaambia mashabiki wake
kuwa hiyo video ni moja wapo ya zawadi kwa mashabiki wake na wapenda
muziki wake pia, video hiyo ikiwa chini ya Director Nisher kutoka Arusha
itakuwa kwenye vituo mbali mbali vya televishen hivi karibuni Alisema
Msanii Roma Mkatoliki.