DADA YAKE DIAMOND ATANGAZA NDOA

 Dada yake msanii Diamond Platnumz, Esma Abdul, amesema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya harusi ya Diamond ambae anatarajiwa kumuoa VJ Penny.
Esma ambae anaishi nyumba moja na kaka yake amesema, “Tumemkubali sana wifi yetu na tunampenda kwa sababu mtu yeyote mimi nitakaetambulishwa siwezi nikamkataa, manake nikimuingilia kwenye mapenzi yake na yeye ataniingilia kwenye mapenzi yangu.”

Huu ni mwezi wa tano toka Esma amjue wifi yake ambae ni Penny, anasema nyumbani amekubalika na mipango ya harusi inaandaliwa japo hajui ni lini itafanyika, manake hiyo ni siri kwa sasa.
Dada yake Diamond aka wifi yake Penny
Zaidi ya wiki tano zilizopita, Diamond aliongea na kusema ndoa yake imekaribia kufungwa na huyo mkewe mtarajiwa ambae ni mjamzito lakini pia akat
hibitisha kumnunulia gari la kutembelea aliloliagiza nchini Japan – Hyundai IX 35.

Mpaka sasa Mwimbaji Diamond Platnums ambae aliongoza kwa kuwa msanii wa Tanzania alieandikwa sana kwenye internet 2012, ameshaingia kwenye headlines za kuwa mapenzini na mastaa wa kike Tanzania kipindi cha nyuma kama Jokate, Wema Sepetu na wengine.

Previous
Next Post »