Baada ya siku kadhaa kupita toka wakali wa Bongo fleva kushirikiana na kudondosha ngoma ya pamoja kati ya Ney na Diamond na ngoma hiyo kufanya vyema katika vyombo vya habari mbalimbali sasa wakali hao wamepanga kuzindua kichupa chao hicho cha Muziki gani siku ya ijumaa ya Tarehe 18 katika ukumbi wa Dar Live pande za Mbagala.
Kama ambavyo track hiyo iliyojaa majigambo katika pande zote mbili kati ya Hip Hop na Rnb siku hiyo wanataka kuona kuwa ni upande upi utafanya poa zaidi jukwaani na kuwadatisha mashabiki,kwani kwa upande wa Diamond ana Hits kibao na upande wa Ney ana Ngoma kali kibao hivyo najiuliza nani atakaa siku hiyo.
Kwa mujibu wa Diamond anatarajia kuupeleka baadaye uzinduzi huo mikoa ya Morogoro, Dodoma, Mwanza na baadaye Arusha akiungana na Mratibu wa onyesho hilo la uzinduzi wa ngoma hiyo.