Baada ya Dully kuondoka, Ngwea aliamua kumuuliza Chidi (ambae mara
nyingi huitana Dogo lao), inakuaje unamzingua kubwa lao, ndipo Chidi
alipopaniki na kuanza kutoa lugha chafu huku akitaka kutokumsikiliza
Ngwea, inasemekana Ngwea aliamua kukaa kimya lakini Chidi aliendelea
kungea kwa hasaira na kusema "ndio nimemzingua kwani yeye nani" na
kumbadilikia Ngwea ambae pia aliamua kuachana nae na kurudi ndani kwenye
meza aliyokua amekaa na washkaji zake,
haikuishia hapo Chidi amkamfata kwenye meza hiyo na kuanza kumuongelea
mbaya Ngwea, na ndipo Ngwea akaamua kushuka chini ya jengo kwa nia ya
kuondoka.
akiwa huko huko chini Chidi alimfata na kumpiga, ikiwa ni pamoja na
kumkata na chupa mkononi,na kupelekwa hospitali ambapo alitibiwa.
nimeongea na Ngwea ambae anasema haoni chochote kilichomfanya kupigwa na msanii huyo.
Ngwea kwa sasa yupo katika kituo cha polisi Oystabay kwa ajili ya
kumfungua mashtaka, licha ya kuumizwa pia ni kutokana na vitisho
alivyopewa na Benzi.
Sio mara ya kwanza kwa Chidi kupiga wasanii wenzake, kama unakumbuka alishawahi kumpiga Matonya na wengine kadhaa.