Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’
huenda akaingia matatani baada ya juzi kupanda jukwaani kutumbuiza
katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 akiwa amevaa sare ya Jeshi la
Wananchi Tanzania (JWTZ), kinyume cha sheria.
Mjadala umeibuka kwa wengi wao kujiuliza nini
maana yake na kama alifanya hivyo kwa kibali maalumu au la, hasa
ikizingatiwa ni hivi karibuni Jeshi hilo lilitoa onyo kwa wasanii na
wengineo kutotumia mavazi hayo.