MISS RED 2014 SITTI ABBAS MTEMVU AVUA TAJI RASMI NA KUMKABIDHI MSHINDI WA PILI TAJI HILO


 Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi na mshindi wa pili, Lillian Kamazima (kulia) aliyechukua nafasi yake pamoja na mshindi wa tatu, Jihhan Dimachk.Sitti Abas Mtemvu amelivua taji hilo baada ya kuiandikia barua Kamati ya Miss Tanzania, November 5 mwaka huu, kuhusiana na uamuzi wake huo.Mrembo huyo alikuwa akikabiliwa na shutuma za kudanganya umri wake, jambo ambalo lilililazimu Baraza la Sanaa la Taifa, (Basata) kutokana na agizo la wizara husika kufuatilia ukweli wake.
                                                        

                                           
         “Napenda niwashukuru wale wote waliokuwa wakinipa sapoti tangu mwanzo nilipoingia katika mashindano haya katika ngazi ya taifa, na warembo wote wa Chang’ombe, Temeke pamoja na wote tuliokuwa nao katika fainali za Taifa. Pia napenda kutuma shukrani za dhati kwa waandaji wote wa kituo cha Chang’ombe, Temeke na wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania kwa mafunzo mbalimbali niliyopata. Nawashukuru pia waandishi wote kwa mchango wenu, pamoja na wizara ya habari, utamaduni na michezo na Baraza la Sanaa kwa busara zenu.”

“Leo nalivuta taji rasmi nililopewa na binadamu lakini alilonipa mwenyezi Mungu bado analo. Mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa uamuzi huo niliochukua.”  
                       
                                                            Lilian Kamanzima
 Mshindi wa pili Miss Reds 2014 ambaye amechukuwa taji la Miss Reds 2014 baada ya kuvuliwa na aliyekuwa mshindi wa kwanza Sitti Abbas Mtemvu.














Previous
Next Post »