QJ KUSAHAU KABISA MASHAIRI YA MUZIKI WA BONGO FLAVA
Mwana muziki wa miondoko ya RNB na Bongo Flava Nchini Tanzania almaarufu kwajina la kisanii QJ ambaye alikuwa katika kundi la WAKALI KWANZA likiongozwa na Mack Mua Na Joslyn kundi ambalo lilifanya vizuri sana kwenye game ya Bongo Flava kipindi cha nyuma, QJ kwasasa amejikita zaidi kwenye muziki wa Injili na kutojihusisha kabisa na muziki wa Bongo Flava, Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo Cha EATV, QJ amesema hakuna kitu kikubwa alichokifanya kwenye muziki kama vitu ambavyo anaviandaa kwa sasa kwaajili ya muziki wa Kumuimbia Mungu zaidi, Baadhi ya Mashairi pia ameshayasahau kwasasa na msanii huyo amesema kuwa kila akikumbuka ya nyuma aliyokuwa akifanya anahisi kuwa anarudi kwenye kuumiza vidonda tu...hivyo msanii QJ tusitegemee kumuona tena kwenye Game ya Bongo Flava ila kwenye muziki wa Injili zaidi.