dickso msami
Msanii Linex ambaye anatamba na ngoma ya 'Aifola' amesema yuko mbioni
kuachia ngoma yake mpya ya mwaka 2013 ambayo humo ndani ameimba kwa lugha 4
tofauti tofauti.Linex alisema kuwa ngoma hiyo mpya ameimba kwa lugha ya
Kiswahili,Kiha,Kiganda na Kiingereza.Linex alisema kuwa ngoma hiyo
imefanywa na Fundi Samwel ambaye kapiga mixing huko Sweden na vocal
amefanya na Tudd Thomas.Linex alisema kuwa pamoja na kwamba Produza Fundi
Samwel hayuko nchini lakini aliingia mkataba nae wakufanya nae kazi na
alisaini kabla produza huyo hajaondoka kurudi kwao Sweden.