KESI YA LULU:WANASHERIA KUOMBA DHAMANA
Msanii wa Filamu za kibongo *Elizabeth Michael *alias Lulu baada ya kipindi
cha nyuma kurudishwa rumande kwa kesi yake inayomkabili kwa kutuhumiwa
kumuua msanii mwenzake,The Late Steven Kanumba,sasa taarifa ambayo
tumeipata ni kwamba wanasheria wake ambao ni Peter kibatala na Kennedy
Fungamtama na Fulgence Massawe wametuma maombi ya dhamana ya kesi ya Lulu
ili isomwe haraka kwasababu muombaji amekaa muda mrefu mahabusu.
Wanasheria hao baada ya kuwasilisha maombi hayo katika mahakama Kuu
wanatarajia kesi hiyo kusikilzwa tena siku ya tarehe 25 mwazi huu mbele ya
Jaji *Zainabu Mruke*..